Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Lot: Priests and Levites designated by, for sanctuary service

27 mistari · 9 vipengele

Mistari kuhusu Priests and Levites designated by, for sanctuary service

  1. Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

  2. Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

  3. Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu, ya pili Yedaya,

  4. ya tatu Harimu, ya nne Seorimu,

  5. ya tano Malkiya, ya sita Miyamini,

  6. ya saba Hakosi, ya nane Abiya,

  7. ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania,

  8. ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu,

  9. ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu,

  10. ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri,

  11. ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi,

  12. ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Yehezkeli,

  13. ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli,

  14. ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

  15. Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

  16. Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki: Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli; kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.

  17. Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe: Ishia alikuwa wa kwanza.

  18. Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi, kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.

  19. Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

  20. Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika; kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.

  21. Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia; na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.

  22. Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.

  23. Wana wa Merari: kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.

  24. Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

  25. Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi: alikuwa Yerameeli.