Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Long-Suffering of God

8 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Bwana akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali.

  2. Hivyo Bwana akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.

  3. Katika dhiki yake akamsihi Bwana Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.

  4. Naye alipomwomba, Bwana akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza kilio chake, kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba Bwana ndiye Mungu.

  5. Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’

  6. kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi.

  7. Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua.

  8. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.