Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Pleasure: Worldly

40 mistari · 1 kipengele

Mistari kuhusu Worldly

Chuja kwa kitabu
  1. “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,

  2. ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.

  3. Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.

  4. Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.

  5. Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.

  6. Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi.

  7. Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani.

  8. “Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”

  9. Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

  10. Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.

  11. Ndipo nilipojitahidi kufahamu kutofautisha hekima, wazimu na upumbavu, lakini nikatambua hata hili nalo ni kukimbiza upepo.

  12. Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili.

  13. Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?”

  14. Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.

  15. Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu.

  16. Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda.

  17. Nikajenga mabwawa ya kukusanya maji ya kunyweshea hii miti iliyokuwa inastawi vizuri.

  18. Nikanunua watumwa wa kiume na wa kike na watumwa wengine walizaliwa nyumbani mwangu. Pia nilikuwa na makundi ya ngʼombe, kondoo na mbuzi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi Yerusalemu kabla yangu.

  19. Nikajikusanyia fedha na dhahabu, hazina za wafalme na za majimbo. Nikajipatia waimbaji wanaume na wanawake, nazo nyumba za masuria: vitu ambavyo moyo wa mwanadamu hufurahia.

  20. Nikawa maarufu sana kuliko mtu mwingine yeyote aliyepata kuishi Yerusalemu kabla yangu. Katika haya yote bado nikawa nina hekima.

  21. Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani, hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu. Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.

  22. Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo mikono yangu ilikuwa imefanya na yale niliyotaabika kukamilisha, kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo; hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.

  23. Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima, wazimu na upumbavu. Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?

  24. Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu, kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

  25. Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo.