Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Noph

13 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri.

  2. Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesi wamevunja taji ya kichwa chako.

  3. Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:

  4. “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, hubiri pia katika Memfisi na Tahpanhesi: ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’

  5. Kwa nini mashujaa wako wamesombwa na kupelekwa mbali? Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana atawasukuma awaangushe chini.

  6. Watajikwaa mara kwa mara, wataangukiana wao kwa wao. Watasema, ‘Amka, turudi kwa watu wetu na nchi yetu, mbali na upanga wa mtesi.’

  7. Huko watatangaza, ‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu, amekosa wasaa wake.’

  8. “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote, “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, kama Karmeli kando ya bahari.

  9. Funga mizigo yako kwenda uhamishoni, wewe ukaaye Misri, kwa kuwa Memfisi utaangamizwa na kuwa magofu pasipo mkazi.

  10. “ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

  11. Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi

  12. Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu, ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi.

  13. Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.