Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Ignorance: General references

46 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. “Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?

  2. Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini?

  3. “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? Ufahamu unakaa wapi?

  4. Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

  5. “Ni wapi basi hekima itokako? Ufahamu hukaa wapi?

  6. Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

  7. Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?

  8. Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?

  9. Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha.

  10. Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili.

  11. Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke

  12. wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.

  13. Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.

  14. (Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;

  15. mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)

  16. Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:

  17. “Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.

  18. Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!

  19. Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.

  20. Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.

  21. Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!

  22. Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.

  23. Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

  24. Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.

  25. Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,