Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Guest

16 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako,

  2. na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi.

  3. Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

  4. Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu,

  5. kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe.

  6. Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.

  7. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu;

  8. ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako

  9. “Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’

  10. Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia.

  11. Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.

  12. Alipoona jinsi wageni walivyokuwa wanachagua mahali pa heshima wakati wa kula, akawaambia mfano huu:

  13. “Mtu akikualika arusini, usikae mahali pa mgeni wa heshima kwa kuwa inawezekana amealikwa mtu mheshimiwa kuliko wewe.

  14. Kama mkifanya hivyo yule aliyewaalika ninyi wawili atakuja na kukuambia, ‘Mpishe huyu mtu kiti chako.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kukaa katika nafasi ya chini kabisa.

  15. Badala yake, unapoalikwa, chagua nafasi ya chini, ili yule mwenyeji wako atakapokuona atakuja na kukuambia, ‘Rafiki yangu, nenda kwenye nafasi iliyo bora zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wenzako wote.

  16. Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”