Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Fool

36 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.

  2. “Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.

  3. Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.

  4. Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa.

  5. Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,

  6. akiita wale wapitao karibu, waendao moja kwa moja kwenye njia yao.

  7. Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”

  8. “Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”

  9. Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

  10. Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.

  11. Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.

  12. Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

  13. Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.

  14. Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.

  15. Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

  16. Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia.

  17. Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.

  18. Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.

  19. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

  20. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!

  21. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.

  22. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.

  23. Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.

  24. Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.

  25. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.