Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Commerce: Increased the wealth of nations and individuals

8 mistari · 64 vipengele

Mistari kuhusu Increased the wealth of nations and individuals

  1. Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni.

  2. Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara baharini zilizoendeshwa na watu wa Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.

  3. Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia.

  4. Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.

  5. Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

  6. Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

  7. Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

  8. Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.