Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Civil Officer

32 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);

  2. Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;

  3. Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;

  4. Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;

  5. Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.

  6. Lakini Solomoni hakumfanya yeyote wa Waisraeli kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa wapiganaji wake, maafisa wake wa serikali, maafisa wake, wakuu wake, majemadari wa jeshi wa magari yake ya vita na wapanda farasi.

  7. Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.