Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Balaam

29 mistari · 8 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa mshahara wa uovu.

  2. Lakini kwa ajili ya uovu wake, alikemewa na punda, mnyama asiyejua kusema, akaongea akitumia sauti ya mwanadamu na kuzuia wazimu wa huyo nabii.

  3. “Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa kafara kwa sanamu na kufanya uasherati.

  4. Vivyo hivyo unao wale wayashikayo mafundisho ya Wanikolai.