Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Astronomy: General references

17 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu General references

  1. “Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? Waweza kulegeza kamba za Orioni?

  2. Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, au kuongoza Dubu na watoto wake?

  3. Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?

  4. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.

  5. Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

  6. Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki.

  7. Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,

  8. linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake.

  9. Huchomoza upande mmoja wa mbingu, na kufanya mzunguko wake hadi upande mwingine. Hakuna kilichojificha joto lake.

  10. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  11. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  12. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.

  13. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.

  14. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.

  15. Hili ndilo asemalo Bwana, yeye aliyeweka jua liwake mchana, yeye anayeamuru mwezi na nyota kungʼaa usiku, yeye aichafuaye bahari ili mawimbi yake yangurume; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:

  16. “Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema Bwana, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”

  17. Hili ndilo asemalo Bwana: “Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika na misingi ya dunia chini ikaweza kuchunguzwa, ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyoyatenda,” asema Bwana.