Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Aaron: Lineage of

10 mistari · 27 vipengele

Mistari kuhusu Lineage of

  1. Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

  2. Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.

  3. Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

  4. Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.

  5. Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.

  6. Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.

  7. (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

  8. Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

  9. Amramu alikuwa na wana: Aroni, Mose, na Miriamu. Aroni alikuwa na wana: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

  10. Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.