Skip to content
Zaburi 119:93-117

Zaburi 119:93-117

93
Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
94
Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
95
Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.
96
Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.
97
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.
98
Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima.
99
Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.
100
Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.
101
Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.
102
Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.
103
Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!
104
Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
105
Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
106
Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.
107
Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako.
108
Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.
109
Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.
110
Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.
111
Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.
112
Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.
113
Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.
114
Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.
115
Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
116
Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.
117
Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options