- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Mithali 6:1-19
1
Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine,
2
kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,
3
basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako!
4
Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie.
5
Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.
6
Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima!
7
Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala,
8
lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9
Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini kutoka usingizi wako?
10
Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
11
hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
12
Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu,
13
ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake,
14
ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina.
15
Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula; ataangamizwa mara, pasipo msaada.
16
Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:
17
macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia,
18
moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,
19
shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
Settings