Mithali 31:13-27
13
Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.
14
Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.
15
Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.
16
Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.
17
Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.
18
Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.
19
Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.
20
Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.
21
Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.
22
Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.
23
Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.
24
Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25
Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.
26
Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.
27
Huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu.
Settings