Skip to content
Mithali 22:1-16

Mithali 22:1-16

1
Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi, kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.
2
Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: Bwana ni Muumba wao wote.
3
Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.
4
Unyenyekevu na kumcha Bwana huleta utajiri, heshima na uzima.
5
Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.
6
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.
7
Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.
8
Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.
9
Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.
10
Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma.
11
Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake.
12
Macho ya Bwana hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.
13
Mvivu husema, “Yuko simba nje!” au, “Nitauawa katika mitaa!”
14
Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana atatumbukia ndani yake.
15
Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.
16
Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali, naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options