Hesabu 33:3-15
3
Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,
4
waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
5
Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6
Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7
Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8
Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9
Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10
Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11
Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12
Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13
Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14
Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
15
Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
Settings