Maombolezo 3:32-56
32
Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
33
Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.
34
Kuwaponda chini ya nyayo wafungwa wote katika nchi,
35
Kumnyima mtu haki zake mbele za Aliye Juu Sana,
36
kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya?
37
Nani awezaye kusema nalo likatendeka kama Bwana hajaamuru?
38
Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema?
39
Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?
40
Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Bwana Mungu.
41
Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:
42
“Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe.
43
“Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma.
44
Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya.
45
Umetufanya takataka na uchafu miongoni mwa mataifa.
46
“Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu.
47
Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.”
48
Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa.
49
Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu,
50
hadi Bwana atazame chini kutoka mbinguni na kuona.
51
Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.
52
Wale waliokuwa adui zangu bila sababu wameniwinda kama ndege.
53
Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe;
54
maji yalifunika juu ya kichwa changu, nami nikafikiri nilikuwa karibu kukatiliwa mbali.
55
Nililiitia jina lako, Ee Bwana, kutoka vina vya shimo.
56
Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”
Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.
Settings