Ayubu 8:13-18
13
Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
14
Lile analolitumainia huvunjika upesi; lile analolitegemea ni utando wa buibui.
15
Huutegemea utando wake, lakini hausimami; huungʼangʼania, lakini haudumu.
16
Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua, ukieneza machipukizi yake bustanini;
17
huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi katikati ya mawe.
18
Unapongʼolewa kutoka mahali pake, ndipo mahali pale huukana na kusema, ‘Mimi kamwe sikukuona.’
Settings