Skip to content
Ayubu 7:11-21

Ayubu 7:11-21

11
“Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.
12
Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, hata uniweke chini ya ulinzi?
13
Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji, nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu,
14
ndipo wanitisha kwa ndoto na kunitia hofu kwa maono,
15
hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, kuliko huu mwili wangu.
16
Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.
17
“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,
18
kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?
19
Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?
20
Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, Ewe mlinzi wa wanadamu? Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? Je, nimekuwa mzigo kwako?
21
Kwa nini husamehi makosa yangu na kuachilia dhambi zangu? Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options