Ayubu 7:11-16
11
“Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.
12
Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, hata uniweke chini ya ulinzi?
13
Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji, nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu,
14
ndipo wanitisha kwa ndoto na kunitia hofu kwa maono,
15
hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, kuliko huu mwili wangu.
16
Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.
Settings