Rukia maudhui
Ayubu 14:13-17

Ombi la hifadhi ya muda na tumaini la wakati ujao

Ayubu 14:13-17
13
“Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka!
14
Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu.
15
Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.
16
Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu.
17
Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options