Rukia maudhui
Hosea 6:7-11

Usaliti na Ufisadi Vinalaaniwa

Hosea 6:7-11
7
Wamevunja Agano kama Adamu: huko hawakuwa waaminifu kwangu.
8
Gileadi ni mji wenye watu waovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
9
Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu, ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, wakifanya uhalifu wa aibu.
10
Nimeona jambo la kutisha katika nyumba ya Israeli. Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba na Israeli amenajisika.
11
“Pia kwa ajili yako, Yuda, mavuno yameamriwa. “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options