Skip to content
Kumbukumbu 32:19-33

Kumbukumbu 32:19-33

19
Bwana akaona hili, akawakataa, kwa sababu alikasirishwa na wanawe na binti zake.
20
Akasema, “Nitawaficha uso wangu, nami nione mwisho wao utakuwa nini, kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka, watoto ambao si waaminifu.
21
Wamenifanya niwe na wivu kwa kile ambacho si mungu, na kunikasirisha kwa sanamu zao zisizokuwa na thamani. Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa. Nitawafanya wakasirishwe na taifa lile lisilo na ufahamu.
22
Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu, ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti. Utateketeza dunia pamoja na mazao yake, na kuwasha moto katika misingi ya milima.
23
“Nitalundika majanga juu yao na kutumia mishale yangu dhidi yao.
24
Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya, yateketezayo na tauni ya kufisha; nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu, na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini.
25
Barabarani upanga utawakosesha watoto; nyumbani mwao hofu itatawala. Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia, pia watoto wachanga na wazee wenye mvi.
26
Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu.
27
Lakini nilihofia dhihaka za adui, adui asije akashindwa kuelewa, na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; Bwana hakufanya yote haya.’ ”
28
Wao ni taifa lisilo na akili, hakuna busara ndani yao.
29
Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili, na kutambua mwisho wao utakuwa aje!
30
Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja, au wawili kufukuza elfu kumi, kama si kwamba Mwamba wao amewauza, kama si kwamba Bwana amewaacha?
31
Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu, sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri.
32
Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kutoka kwenye mashamba ya Gomora. Zabibu zake zimejaa sumu, na vishada vyake vimejaa uchungu.
33
Mvinyo wao ni sumu ya nyoka, sumu yenye kufisha ya swila.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options