1 Nyakati 8:6-27
6
Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
7
Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
8
Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.
9
Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu,
10
Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.
11
Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12
Wana wa Elpaali walikuwa: Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka),
13
na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14
Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi,
15
Zebadia, Aradi, Ederi,
16
Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17
Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,
18
Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
19
Yakimu, Zikri, Zabdi,
20
Elienai, Silethai, Elieli,
21
Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22
Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,
23
Abdoni, Zikri, Hanani,
24
Hanania, Elamu, Anthothiya,
25
Ifdeya na Penueli.
26
Shamsherai, Sheharia, Athalia,
27
Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
Settings