Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Timbrel

9 mistari · 4 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza.

  2. Yefta aliporudi nyumbani Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.

  3. Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.

  4. Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

  5. Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi.

  6. Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, pamoja nao wako wanawali wakipiga matari.

  7. Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.

  8. Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

  9. msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,