Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribe Of Manasseh: Half of, obtained inheritance east of Jordan

7 mistari · 30 vipengele

Mistari kuhusu Half of, obtained inheritance east of Jordan

  1. Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.

  2. Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.

  3. Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.

  4. Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

  5. Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo:

  6. Eneo lililoenea kuanzia Mahanaimu, na kujumlisha Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini,

  7. nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.