Mistari ya Biblia kuhusu The Roman Empire: Use of the panoply or defensive armour
Mistari kuhusu Use of the panoply or defensive armour
Usiku umeendelea sana, mapambazuko yamekaribia. Kwa hiyo tuyaweke kando matendo ya giza na tuvae silaha za nuru.
katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi.
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani,
nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani.
Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.