Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Feast of Tabernacles: Singing hosannas

6 mistari · 17 vipengele

Mistari kuhusu Singing hosannas

  1. Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake.

  2. Ee Bwana, tuokoe, Ee Bwana, utujalie mafanikio.

  3. Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.

  4. Bwana ndiye Mungu, naye ametuangazia nuru yake. Mkiwa na matawi mkononi, unganeni kwenye maandamano ya sikukuu hadi kwenye pembe za madhabahu.

  5. Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

  6. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.