Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Call of God

47 mistari · 33 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  2. Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,

  3. kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.

  4. Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona!

  5. Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; hujivizia tu wenyewe!

  6. Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila; huuondoa uhai wa wale wenye mali.

  7. Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;

  8. kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:

  9. “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa?

  10. Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu.

  11. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu,

  12. kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

  13. mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  14. wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

  15. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.

  16. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,

  17. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  18. watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.

  19. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.

  20. Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu,

  21. nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza),

  22. ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”

  23. Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Bwana Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana.

  24. “ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  25. ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”