Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Science: Observations of, and deductions from, facts

13 mistari · 3 vipengele

Mistari kuhusu Observations of, and deductions from, facts

  1. Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.

  2. Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

  3. Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake.

  4. Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza.

  5. Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.

  6. Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.

  7. Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

  8. Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”

  9. Nilitumia muda wangu wote kujifunza na kuvumbua kwa hekima yote yanayofanyika chini ya mbingu. Jinsi gani Mungu ameweka mzigo mzito juu ya wanadamu!

  10. Nimeshaona mambo yote yanayotendeka chini ya jua, hayo yote ni ubatili, hii ni kukimbiza upepo.

  11. Kilichopindika hakiwezi kunyooshwa, kile ambacho hakipo haiwezekani kukihesabu.

  12. Niliwaza mwenyewe, “Tazama, nimekua na kuongezeka katika hekima kuliko yeyote aliyewahi kutawala Yerusalemu kabla yangu. Nimekuwa na uzoefu mkubwa wa hekima na maarifa.”

  13. Ndipo nilipojitahidi kufahamu kutofautisha hekima, wazimu na upumbavu, lakini nikatambua hata hili nalo ni kukimbiza upepo.