Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Legends

7 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.

  2. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

  3. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.

  4. Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

  5. Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu.

  6. Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo.

  7. Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu,