Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Continents

26 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo.

  2. Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

  3. Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko.

  4. Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.

  5. Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote.

  6. Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.

  7. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.

  8. Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

  9. Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

  10. wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?

  11. “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo,

  12. nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene,

  13. nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

  14. niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?

  15. “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

  16. yapate kushika miisho ya dunia, na kuwakungʼuta waovu waliomo?

  17. Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri; sura yake hukaa kama ile ya vazi.

  18. Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.

  19. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?

  20. Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti? Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?

  21. Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote.

  22. Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.

  23. Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.

  24. Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

  25. yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.