Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Christian Conduct: Blessedness of maintaining

16 mistari · 48 vipengele

Mistari kuhusu Blessedness of maintaining

  1. Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

  2. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  3. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.

  4. Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.

  5. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

  6. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  7. “Heri walio maskini wa roho, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

  8. Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

  9. Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi.

  10. Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

  11. Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.

  12. Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

  13. Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

  14. Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

  15. “Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu.

  16. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.