Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Ambition: Vanity of

15 mistari · 22 vipengele

Mistari kuhusu Vanity of

  1. macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.

  2. Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu,

  3. ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’

  4. Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.

  5. Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena.

  6. Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.

  7. Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.

  8. Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.

  9. Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari.

  10. Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake.

  11. Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,

  12. kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.

  13. Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,

  14. atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.

  15. Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.