Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Nyakati 29:1takriban 1015 KK

    Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili ya Bwana.

  2. 1 Nyakati 29:2takriban 1015 KK

    Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno.

  3. 1 Nyakati 29:3takriban 1015 KK

    Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu:

  4. 1 Nyakati 29:4takriban 1015 KK

    talanta 3,000 za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000 za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu,

  5. 1 Nyakati 29:5takriban 1015 KK

    kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?”

  6. 1 Nyakati 29:6takriban 1015 KK

    Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

  7. 1 Nyakati 29:7takriban 1015 KK

    Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000 na darkoni 10,000 za dhahabu, talanta 10,000 za fedha, talanta 18,000 za shaba na talanta 100,000 za chuma.

  8. 1 Nyakati 29:8takriban 1015 KK

    Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni.

  9. 1 Nyakati 29:9takriban 1015 KK

    Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

  10. 1 Nyakati 29:10takriban 1015 KK

    Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema: “Uhimidiwe wewe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, tangu milele hata milele.

  11. 1 Nyakati 29:11takriban 1015 KK

    Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee Bwana, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

  12. 1 Nyakati 29:12takriban 1015 KK

    Utajiri na heshima vyatoka kwako; wewe ndiwe utawalaye vitu vyote. Mikononi mwako kuna nguvu na uweza ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

  13. 1 Nyakati 29:13takriban 1015 KK

    Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kulisifu Jina lako tukufu.

  14. 1 Nyakati 29:14takriban 1015 KK

    “Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako.

  15. 1 Nyakati 29:15takriban 1015 KK

    Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini.

  16. 1 Nyakati 29:16takriban 1015 KK

    Ee Bwana Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako.

  17. 1 Nyakati 29:17takriban 1015 KK

    Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.

  18. 1 Nyakati 29:18takriban 1015 KK

    Ee Bwana, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako.

  19. 1 Nyakati 29:19takriban 1015 KK

    Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

  20. 1 Nyakati 29:20takriban 1015 KK

    Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini Bwana Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za Bwana na mfalme.

  21. 1 Nyakati 29:21takriban 1015 KK

    Siku ya pili yake wakamtolea Bwana dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli.

  22. 1 Nyakati 29:22takriban 1015 KK

    Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.

  23. 1 Nyakati 29:23takriban 1015 KK

    Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii.

  24. 1 Nyakati 29:24takriban 1015 KK

    Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.

  25. 1 Nyakati 29:25takriban 1015 KK

    Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.