Rukia maudhui

Jesus

3,872 mistari · 6 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Jesus Christ, Immanuel, Emmanuel, Christ

Mistari inayomtaja Jesus

Chuja kwa kitabu
  1. Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.

  2. “Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake.

  3. “Mimi siwezi kufanya jambo lolote peke yangu. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake yeye aliyenituma.

  4. “Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.

  5. Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli.

  6. Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa.

  7. “Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma.

  8. Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,

  9. wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye.

  10. Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.

  11. Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.

  12. “Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu.

  13. Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.

  14. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.

  15. “Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu.

  16. Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu.

  17. Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”

  18. Baada ya haya, Yesu alikwenda ngʼambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia.

  19. Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa.

  20. Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.

  21. Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”

  22. Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.

  23. Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”

  24. Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,

  25. Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000.