Skip to content
Ufunuo 2:9

Ufunuo 2:9

Inaonyesha mstari 9 pamoja na muktadha unaouzunguka.
6
Lakini una jambo hili kwa upande wako: Unayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo nami pia nayachukia.
7
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa haki ya kula matunda toka kwa mti wa uzima, ambao uko katika paradisoya Mungu.
8
“Kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa kisha akafufuka.
9
Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali wao ni sinagogi la Shetani.
10
Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
11
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa kamwe na mauti ya pili.
12
“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Pergamo andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 90 chars

Options