Zaburi 80:8-19
8
Ulileta mzabibu kutoka Misri, ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9
Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
10
Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
11
Matawi yake yalienea mpaka Baharini, machipukizi yake mpaka kwenye Mto.
12
Mbona umebomoa kuta zake ili wote wapitao karibu wazichume zabibu zake?
13
Nguruwe mwitu wanauharibu na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
14
Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu,
15
mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, mwana uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
16
Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, unapowakemea, watu wako huangamia.
17
Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
18
Ndipo hatutakuacha tena, utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
19
Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa.
Settings