Zaburi 73:12-22
12
Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.
13
Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.
14
Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.
15
Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.
16
Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.
17
Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.
18
Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu.
19
Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!
20
Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.
21
Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22
nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
Settings