Skip to content
Zaburi 136:14-26

Zaburi 136:14-26

14
Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.
15
Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.
16
Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele.
17
Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.
18
Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.
19
Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele.
20
Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele.
21
Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele.
22
Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele.
23
Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele.
24
Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele.
25
Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele.
26
Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.

Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.

Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options