Zaburi 136:16-22
16
Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele.
17
Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.
18
Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.
19
Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele.
20
Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele.
21
Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele.
22
Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele.
Settings