Zaburi 136:10-15
10
Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele.
11
Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.
12
Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.
13
Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.
14
Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.
15
Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.
Settings