Zaburi 106:27-38
27
kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote.
28
Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.
29
Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao.
30
Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa.
31
Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.
32
Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao;
33
kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.
34
Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza,
35
bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao.
36
Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao.
37
Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani.
38
Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
Settings