Zaburi 106:13-33
13
Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake.
14
Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani.
15
Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.
16
Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.
17
Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake.
18
Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu.
19
Huko Horebu walitengeneza ndama, na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.
20
Waliubadilisha Utukufu wao kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.
21
Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,
22
miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.
23
Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.
24
Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake.
25
Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana.
26
Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani,
27
kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote.
28
Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.
29
Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao.
30
Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa.
31
Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.
32
Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao;
33
kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.
Settings