Mithali 29:8-14
8
Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
9
Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10
Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11
Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.
12
Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.
13
Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
14
Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
Settings