Mithali 29:1-7
1
Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa.
2
Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
3
Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
4
Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
5
Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake.
6
Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
7
Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.
Settings