Rukia maudhui
Mithali 27:17-22

Kukuzana na Asili ya Mwanadamu

Mithali 27:17-22
17
Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
18
Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
19
Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.
20
Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu.
21
Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.
22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options