Mithali 22:17-34
17
Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,
18
kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.
19
Ili tumaini lako liwe katika Bwana, hata wewe, ninakufundisha leo.
20
Je, sijakuandikia misemo thelathini, misemo ya mashauri na maarifa,
21
kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, ili uweze kutoa majibu sahihi kwake yeye aliyekutuma?
22
Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, wala kumdhulumu mhitaji mahakamani,
23
kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao naye atawateka wao waliowateka.
24
Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,
25
la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.
26
Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.
27
Kama ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia.
28
Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani lililowekwa na baba zako.
29
Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? Atahudumu mbele ya wafalme; hatahudumu mbele ya watu duni.
Settings