Hesabu 32:34-42
34
Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri,
35
Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha,
36
Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo.
37
Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,
38
pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.
39
Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.
40
Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.
41
Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.
42
Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.
Settings